Kampuni ya Apple inatarajiwa kuzindua simu zake mpya za iPhone 7 Jumatano hii huko San Francisco, California.
Simu hiyo inatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya ile ya iPhone 6 huku wengi wakipendelea kuona simu hizo zisiwe na tundu la kutumia headphone jack na badala yake ziwe na uwezo wa kutumia teknolojia ya Bluetooth au kutumia Lightning ambalo pia hutumiwa kuweka chaji.
Aidha simu hizo mpya za iPhone 7 zinatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kamera na huenda simu hizo zikawa na lens mbili za kamera ambazo zitamwezesha mtumiaji kupiga picha za ubora wa hali ya juu.
Uzinduzi huo unafanyika ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mpinzani mkubwa wa kampuni hiyo ambayo ni kampuni ya Samsung kulazimika kusitisha uuzaji wa simu yake ya kisasa zaidi ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri.
Hata hivyo wachunguzi bado wanaendelea kujadiliana kama vifaa vilivyotumika kutengenezea simu hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa kama havitaleta madhara kama ilivyokuwa kwenye Galaxy Note 7.
0 comments:
Post a Comment